Advertise your ,university, college,schools, books
and any other materials for studies through our elimumedia.blogspot.com
0713765905/0768805151
0713765905/0768805151
Monday, April 10, 2017
HISTORIA FUPI YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE. RAISI NA MUASISI WA KWANZA WA TANZANIA.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mnamo tarehe13 April 1922 na alifariki 14 October 1999. Akiwa ni Mtanzania wa kwanza kujitolea katika nyazifa za uongozi kuwasaidia Watanzania. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa kutoka katika familia ya Chifu Burito Nyerere wa kabila za Wazanaki. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alijulikana kwa jina la mwalimu kutokana na kazi yake ya ualimu. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara . Alikuwa mtoto wa 26 katika familia ya Chifu Burito
. Chifu Burito Nyerere alizaliwa mwaka 1860 na alifariki mwaka 1942. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianza shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 12 na baadae alifaulu kwenda sekondari katika shule ya sekondari Tabora. Baada ya elimu yake ya sekondari alichaguliwa kwenda chuo cha Makerere nchini Uganda alipopata elimu yake ya stashahada(Diploma). Baada ya kuhitimu elimu yake nchini Uganda alirudi nchini Tanzania (Tanganyika)na kukaa kwa miaka 3 akifanya kazi ya kufundisha katika shule ya sekondari ya mtakatifu mary (S.t Mary’s secondary School) mkoani Tabora katika masomo ya sayansi na kiingereza (Biology and English). Mnamo mwaka 1949 alichaguliwa kwenda nchini Uingereza chuo kikuu cha Edinburgh (University of Edinburgh) katika masomo yake ya shahada na shahada ya uzamili katika masomo ya sanaa na uchumi na historia.
Akiwa nchini Uingereza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikutana na mtanzania mwenzake aliyefahamika kwa jina la Fabian na hapo walishauriana na kuendeleza mapambano dhidi ya kuikomboa Tanganyika kutoka mikononi mwa mkoloni Mwingereza na kuiunganisha na sera ya kijamaa ya nchi za mashariki ya mbali kama vile China na Russia. Baada ya kurudi nchini Tanzania mwaimu Julius Kambarage Nyerere aliendelea kufundisha katika shule ya Mtakatifu Francis (S.t Francis’ College) kwa sasa ikijulikana kwa jina la Pugu Sekondari iliyopo jijini Dar es salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa Raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA).
Mwaka 1954 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikiunda upya chama cha TAA na kukipa jina la Tanganyika African National Union (TANU)akiwa na dhumuni kuu la kuikomboa nchi ya Tanganyika kupitia chama hicho na sera kuu ya chama ilikuwa ni kuikomboa nchi kutoka kwa Waingereza. Chama cha TANU kilisajili wanachama wapya wengi zaidi ili kuiwezesha kirahisi kupigania uhuru wa nchi. Kwa juhudi kubwa na ukomavu aliokuwa nao kisiasa katika kuikomboa nchi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliwashtua sana wakoloni na serikali yao. Hivyo walimtaka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere achague kati ya kufundisha au kuwa mwanasiasa. Mwalimu J.K Nyerere alimua kuacha ualimu na kuendelea na siasa akiwa na lengo la kuikomboa nchi ya Tanganyika toka minyororo ya unyonyaji na udhalimu wa wakoloni na kuwa taifa huru litakalojiendesha kisiasa ,kiuchumi,kijamii na kiutamaduni. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimua kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya Mawasiliano katika kampeni zake zote alipopita kuwahutubia wanachi wa Tanganyika(Tanzania) Mwalimu Julius kambarage nyerere alihudhuria mikutano mbalimbali ya kimataifa nje na ndani ya nchi. Jitihada zake zote hizi zilimsaidia kwa kiasi kikubwa kukifanya chama cha TANU kipate wafuasi wengi. Kiongozi mmoja katika kikoloni serikali ya kikoloni aliyefahamika kwa jina la Sir Richard Turnbull aliguswa na jitihada za Mwalimu Julius J.K.Nyerere na kuanza kumsaidia katika jitihada zake za kulikomboa Taifa katika mikono dhalimu ya wakoloni. Mwaka 1958 -59 Mwalimu J.K Nyerere alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika serikali ya kikoloni . Kufikia mwaka 1960 Tanganyika iliandaliwa kujipatia uhuru wake kupitia mataifa mbalimbali yaliyokuwa yakiisaidia Tanganyika kupigania uhuru(Urusi,Umoja wa mataifa,China n.k) na tarehe 9 Desemba 1961 Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni Mwiingereza na Mwalimu J.K Nyerere akiwa waziri mkuu wa kwanza kuiongoza nchi ya Tanganyika kabla ya kuwa Jamuhuru mwaka 1962.
Baada ya nchi Tanganyika kuwa Taifa huru na kuwa Jamhuri mwaka 1962 Mwalimu J.K. Nyerere alikuwa Raisi wa kwanza wa Tanganyika na muasisi wa Taifa hili mpaka mwaka 1985 alipomchagua Raisi Ally Hassan Mwinyi kuwa mrithi wake kupitia chama cha mapinduzi(C.CM). Mwaka 1964 Mwalimu J.K. Nyerere aliiunganisha nchi ya Tanganyika na visiwa vya Zanzibar baada ya visiwa hivi kuwa huru toka kwa Sultan Jamshid bin Abdullah chini kiongozi Abeid Amani Karume. Kiongozi Abeid Amani Karume akishirikiana na kiongozi wa kivita aitwaye ndugu John Okello toka nchini Uganda walifanikiwa kuvikomboa visiwa vya Zanzibar toka chini ya utawala wa kidhalimu wa waarabu INAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO………………………..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment